Wednesday, October 10, 2012

Waziri Mkuu, Mkuu Mizengo Pinda Alipokutana na wajumbe wa Kituo cha

Waziri Mkuu, Mkuu Mizengo Pinda akiwa na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia (TCD) baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake jijini Dar es salaam Oktoba 8, 2012. Wejumbe hao ni viongoazi wa vyama mbali mbali vya siasa nchini.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
 Mwenyekiti wa Tume Ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Jaji Kiongozi (Mstaafu) Amiri Ramadhan Manento (katikati) akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani jijini Dar es Salaam leo wakati akitoa muhtasari wa taarifa ya Uchunguzi wa Tume yake kuhusu tukio lililopelekea kifo cha Daudi Mwangosi kilichokea Septemba 2, 2012 kijijini Nyololo. Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa. (Kushoto) ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mahfoudha.A. Hamid na (kulia) ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Tume hiyo Florida Kazora.
 Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mahfoudha.A. Hamid  akizungumza wakati tume hiyo ilipokutana na waandishi wa habari leo
Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki kwenye mkutano huo.Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO

Monday, October 8, 2012

Ripoti Za Kifo Cha Mwangosi Kuwekwa Hadharani Leo



Na: Elizabeth Edward, Mwananchi.

 SERIKALI leo inatoa hadharani ripoti ya Kamati iliyoundwa kupata taarifa kuhusu vurugu zilizotokea mkoani Iringa na kusababisha kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi. Wakati ripoti hiyo ikitarajiwa kutolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Kamati nyingine iliyoundwa na Baraza la Habari (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tef), nayo leo inatarajiwa kuweka hadharani ripoti yake.

 Kamati hizo ziliundwa kwa nyakati tofauti baada ya vurugu zilizotokea Septemba 2, mwaka huu katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi wakati polisi walipowatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakifungua tawi la chama hicho katika kijiji hicho. 

 Juzi, Makamu Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Dk Nchimbi, Theophil Makunga alimkabidhi waziri huyo na kusema Kamati yake ilifanya ziara Iringa na pia mahojiano na wadau mbalimbali Dar es Salaam.Kamati ya Nchimbi ilikuwa ikiongozwa na Mwenyekiti Jaji Steven Ihema, Makunga na Ofisa wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Pili Mtambalike, Kanali Wema Wapo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) pamoja na Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi, Isaya Mngullu.

Tofauti na taarifa nyingine, ripoti ya mauaji ya Mwangosi inatarajiwa kutolewa hadharani ili umma uweze kuisoma, kuichambua na kutoa maoni kuhusu hatua za kuchukua ili matukio ya aina hiyo yasitokee tena. Ripoti ya MCT Katibu Mkuu wa Tef, Neville Meena alisema timu ya uchunguzi imeshamaliza kazi yake na leo itatoa rasmi ripoti kuhusiana na mazingira ya kifo cha Mwangosi.

Kamati hiyo iliundwa na watu watatu, John Mirenyi kutoka MCT, Hawra Shamte kutoka Tef na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Saimon Berege. “Sisi tukiwa wanahabari tuliunda Kamati yetu ili ifanye uchunguzi kuhusiana na mauaji ya mwanahabari mwenzetu, baada ya kukamilisha uchunguzi huo, sasa tupo tayari kuiwasilisha ripoti yetu hadharani,” alisema Meena. 

Chanzo:  http://www.mwananchi.co.tz

Mtumishi Wa Papa Ahukumiwa Kifungo ha miezi 18 jela





Mtumishi wa zamani wa Papa Benedict amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na nusu kwa kuiba nyaraka za siri kutoka fleti ya Papa. 

Paolo Gabrieli na Papa Benedict Katika kujitetea mbele ya mahakama ya Vatikani, Paolo Gabriele alisema alifichua nyaraka hizo za siri kwa mwandishi wa habari kwa sababu akitaka kuonesha kile alichosema ni rushwa ovu ilioko katikati ya Kanisa la Katoliki. Msemaji wa Vatikani, Federico Lombardi, alieleza kuwa inavoelekea Papa atamsamehe mtumishi wake.

Uzinduzi Kampeni Za Udiwani CHADEMA Arusha


 Mgombea wa CHADEMA
Nassari akihutubia

Maelfu ya wananchi.jana jioni

Ajali Yaua watu Wawili Papohapo


Dereva wa Bodaboda na abiria wake, ambao hawakuweza kufahamika majina yao kwa haraka, wakiwa wamelazwa pembeni mwa barabara ya Bagamoyo eneo la Makongo, baada ya kugongwa na gari aina ya Starlet yenye namba za usajiri T 838 BKB, wakati wakiwa katika Pikipiki yao yenye namba za usajiri T 491 BFY, na kufariki dunia papo hapo. Ajali hiyo ilitokea jana asubuhi, Pichani ni raia akijaribu kutambua mwili wa marehemu katika ajali hiyo.

Sunday, October 7, 2012

Kardinali Rugambwa azikwa mara ya pili Bukoba

Anaonekana Baba Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini mara tu baada ya kukagua gari litakalo tumika kubebe mwili wa marehemu Kardinali Rugambwa
 Muonekano wa ndani ya Gari.
Muonekano wa gari litakalo ubeba mwili wa Marehemu Kardinali Rugambwa likiwa tayari limepambwa Maua.
 Mtangazaji wa kipindi cha dini, TBC katika kuwajibika
 Mzee Dioniz Malinzi akiteta jambo na Askofu Kilaini.
 Kila baada ya muda ndivyo wanavyozidi kuwasili Viongozi mbalimbali wa dini .
 Kikundi cha Ngoma kutoka nchini Burundi kikiendelea  na mashamsham  katika mahadhimisho haya.
 Shamrashamra za hapa na pale zikiendelea.
 Wadau na waumini wakikiristo wakifurahia burudani ya ngoma kutoka Nchini Burundi.

kuelekea ndani ya kanisa kuu.

 Mwili ukiingizwa ndani ya kanisa kuu katoliki Jimbo la Bukoba

 Heshima ya mwisho katika katika ktabaruku mwili wa Kardinali.
 Hapa nashindwa nielezeje ingawa naamini ni mwanzo wa ukurasa mwingine  katika kuendeleza  historia ya Marehemu Kardinal Rugambwa.


Monekano wa kaburi jipya ndani ya kanisa kuu, na pembeni yake zipo kaburi nyingine tatu.

 MISA IMEONGOZWA NA ASKOFU MKUU JIMBO LA MWANZA YDATHADEI RUAICH NA KUSAIDIWA NA NESTORIUS TIMANYWA.


Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda mara tu baada ya kuwasili mjini bukoba
 Watu na matukio,hapa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwajibika
 Watu walioandaliwa maalum wakiwa wamebeba jeneza lililo na masalia ya Kardinali Laurean Rugambwa yatari kuingizwa katika Kanisa Kuu la Jimbo la Bukoba, la Bikira Maria wa Huruma kwa maziko.




Jeneza hilo lilokuwa na masalia likiwa limebebwa juu.

Na Theonestina Juma, Bukoba
MAELFU ya waumini wa Kanisa Katoliki kutoka ndani na nje ya nchi wamejitokeza kushiriki maziko rasmi ya masalia ya Kardinali wa Kwanza Mwafrika,Laurean Rugambwa yaliofanyika jana mjini Bukoba.
Misa ya kuombea masalia ya Kardinali huyo yalioongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza,Mhashamu Jude Thadeus Ruwa'ichi, katika Parokia ya Kashozi alikokuwa amezikwa kwa muda kutokana na Kanisa kuu la Bukoba la Bikira Maria wa Huruma aliloanza kujenga mwenyewe akiwa hai na kutaka azikwe lilikuwa likifanyiwa ukarabati mkubwa uliochukua takribani miaka 10.
Katika misa hiyo ilioendeshwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Jude Thadeus Ruwa’ichi yamehudhuriwa na maaskofu zaidi ya 30 kutoka katika majimbo mbali mbali hapa nchini pamoja na miamia ya mapadri pamoja na watawa
Katika parokia ya Kashozi kutokana na uwingi wa watu waliojitokeza kushiriki katika misa ya ililazimika geti la kuingilia kanisani kufungwa kwa muda kwa kuhofia kungeweza kutokea watu kukanyagana, ambapo geti hilo lilifunguliwa wakati wa kukominika.
"Naomba geti la lango kuu lililokuwa limefungwa lifunguliwe kwani kwa sasa ni wakati wa kukomunika"alisikika Padri mmoja akitoa maelekezo.Akihubiri katika misa hiyo ya kuhamisha masalia ya Kardinali Rugambwa,Mhashamu Ruwa'ichi alisema kila Askofu wa jimbo wa Kanisa hilo wanayo haki ya kuchagua azikwe wapi.
Alisema hata Kardinali Rugambwa angependekeza azikwe Jijini Dar Es Salaam alikofanyia kazi za kiuchungaji kwa miaka mingi ingetekelezwa, lakini kwa hiari na utashi wake alitaka azikwe Bukoba hivyo ni haki yake.
"Kila Askofu anawajibu wa kuchagua azikwe wapi, naye Kardinali Rugambwa alitaka azikwe Katika Kanisa Kuu la Bukoba, ni haki yake na hatimaye leo tunahamisha masalia yake na kwenda kuzika rasmi"alisema Askofu Ruwa'ichi.
Alisema kuhifadhiwa rasmi masalia yake katika kanisa hilo yatakuwa yakiombewa na waumini kutoka katika maeneo mbali mbali kutokana na jinsi alivyokuwa akithamini dini na kumtumikia Mungu.Alisema kupumzishwa si kwamba ni mahali pake bali ni sehemu alikoandaliwa na Mungu.
Alisema kazi kubwa ya Kardinali Rugambwa ilikuwa ni kuwaelekeza watu njia ya kwenda kwa Yesu.
Alisema katika mafundisho hayakuwa porojo bali alieneza habari njema za kumpenda, kumtumikia Mungu.
Hata hivyo baada ya misa hiyo yalianza maandamano ya magari na pikipiki ambayo yaliongozwa na Jeshi la polisi Mkoani Kagera ambapo maandamano hayo yalifika Bukoba mjini saa 9.00 alasiri huku jeneza lililobeba la Masalia yake likiwa la kifahari lenye namba ya usajili,T 607 BYX
Masalia ya Kardinali Rugambwa yaliwekwa karibuni saa 4.20 jioni na watu maalum waliokuwa wameandaliwa.
Aidha katika maziko hayo rasmi katika eneo la kaburi walioenda ni waandishi wa habari, maaskofu na baadhi ya mapadri waliokuwa na shughuli maalum pekee.
Askofu Ruwa’ichi aliwaongoza baadhi ya maaskaofu kuweka mashada ya maua katika kaburi la Kadinali Rugambwa, ambapo katika eneo alikozikwa jumla  kuna makaburi matatu.
Hata hivyo katika mazishi hayo hayakuweza kuwahiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambapo yeye alitua mjini hapa saa 4.30 jioni wakati maziko hayo yalianza saa 9.30 alasiri na saa 4.20 akapumzishwa katika nyumba yake ya milele.
Kutokana na uwingi wa watu waliofurika katika maziko hayo mjini hapa, magari yote yalioamuriwa kwenda kuegeshwa katika uwanja wa Kaitaba kulingana na maelezo yaliotolewa na Jeshi la polisi, ambapo hata watu waliokuwa wakiuza bidhaa mbali mbali walialimika kuuza zaidi ya mita 500 kutoka katika eneo la sherehe hizo.
Katika sherehe za maziko hayo wanaumini waliweza kushudia moja kwa moja kupitia screen za lungina zilizokuwa zimewekwa kila sehemu katika viwanja vya makanisa hayo, Kashozi na Bukoba mjini.
Hata hivyo idadi ya watu waliokuwa nje ya uwanja wa kanisa hilo  waliokosa nafasi ya kukaa ilikuwa sawa na watu waliokuwa ndani ya viwanja vya kanisa hilo.
Kardinali Rugambwa alizaliwa  Julai 12, 1912 katika kijiji cha Bukongo Rutabo Kamachumu wilayani Muleba katika familia ya kifalme na kufariki dunia mwaka 1997 akiwa na miaka 85.

Thursday, October 4, 2012

Meli Ya Utoaji Mimba Yazuiliwa Kuingia Morocco



 
 
 
 
Meli moja ya Uholanzi iliyokuwa ikielekea katika pwani ya Morocco kutoa huduma ya utoaji mimba kwa wanawake imezuiliwa kuingia bandarani kwa mujibu wa wanaharakati walioituma nchini humo. 

Kundi la wanaharakati hao wanawake linasema kuwa bandari ya Smir imefungwa kabisa na meli za kivita zinalinda doria eneo la bandari hiyo.

 Hapo jana Morocco ilisema kuwa meli hiyo haijapewa mualiko na mamlaka zinazotambuliwa nchini humo na hivyo ilikuwa ikifanya shughuli hiyo kinyume cha sheria. Sheria za Morocco zinakataza utoaji mimba isipokuwa tu iwapo maisha ya mwanamke mjamzito yako hatarini. 

 Ibtissame Lachgar, ambaye ni mmoja wa wanaharakati wanaotetea haki ya utoaji mimba amesema wanawake wengi wanalazimika kufanya utoaji mimba kwa njia zisizo rasmi ambazo ni hatari. 

                Chanzo:http://www.bbc.co.uk/swahili/habari

Sumaye atahamia CHADEMA?


Na: Mussa Juma, Arusha na Boniface Meena,MWANANCHI 

SIKU chache baada ya kushindwa katika uchaguzi wa ndani kwenye nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amekutana na viongozi wa Chadema ikidaiwa kuwa ni kujadili pamoja na mengine, uwezekano wa kuhamia huko ili agombee urais katika Uchaguzi Mkuu ujao 2015.

 Sumaye ambaye anatajwa kuwa alikuwa na mpango wa kuwania urais kupitia CCM, alishindwa katika uchaguzi wa kuwania ujumbe wa Nec, baada ya kupata kura 481 dhidi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk Mary Nagu aliyepata kura 648. 

Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wa Chadema, zimeeleza kuwa Sumaye hakuridhishwa na mchakato wa uchaguzi huo wa Nec na kwa matokeo hayo, alikutana na viongozi wa Chadema kujadili mustakabali wake kisiasa. Jana, mjumbe mmoja wa Kamati Kuu ya Chadema, ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, alithibitisha Sumaye kukutana na viongozi wa Chadema.

 Hata hivyo alisema hawajafikia mwafaka. Alisema mawasiliano ya Chadema na Sumaye yalianza mara tu baada ya matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Septemba 30, mwaka huu yaliyomwengua kigogo huyo kwenye kinyang’anyiro hicho.

 “Ni kweli kuna watu wa CCM tumewasiliana nao baada ya uchaguzi ule (wa Nec) na Sumaye tunawasiliana naye pia lakini siwezi kusema tumefikia wapi,” alisema mjumbe huyo na kuendelea: “Suala kwamba amekubaliwa kujiunga na Chadema au la, nadhani huu ni uamuzi wake. Ninachoweza kusema ni kwamba vikao vilikuwepo na vinaendelea kukaliwa.

 Alisema baada ya matokeo ya Hanang’ na hali ya kisiasa ndani ya CCM, Chadema kimekuwa kikiwasiliana na Sumaye na kikubwa ambacho kinajionyesha ni kada huyo wa CCM kutoridhishwa na hali ya mambo ndani ya chama chake. Mjumbe huyo wa Chadema alisema chama hicho Wilaya ya Hanang’ kinaandaa mkutano maalumu wa kuwapokea wanachama wapya wa CCM, wengi wao wakiwa baadhi ya walioanguka kwenye uchaguzi wa Nec wilayani humo. 

Habari zaidi zimeeleza kuwa Chadema kimepanga siku yoyote juma lijalo, kuwapokea wanachama wapya kutoka CCM, baadhi wakiwa wale walioshindwa kwenye uchaguzi wa ndani ya chama hicho uliofanyika wilayani Hanang’. Mmoja wa watu wa karibu na Sumaye alisema anachojua ni kwamba Chadema wanamtaka Sumaye na siyo Sumaye kukitaka chama hicho cha upinzani. 

“Wamekuwa wakimfuatafuata mara nyingi na mazungumzo ya aina hiyo si mageni baina ya Sumaye na Chadema. Ila ninachoweza kusema, safari hii chochote kinaweza kutokea kutokana na hasira alizonazo (Sumaye). Ngoja tusubiri, atafanya mkutano na waandishi Jumapili.” Sumaye, Mbowe wazungumza Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Sumaye alisisitiza kuwa atazungumzia masuala yote yanayohusiana na uchaguzi huo wa Hanang’ atakapokutana na waandishi wa habari, Dar es Salaam.

 “Nitakutana na waandishi wa habari kuzungumzia kilichotokea naomba tu mwendelee kunipa muda,” alisema Sumaye na kuongeza kuwa alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda Dar es Salaam. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema asingependa kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yeye si msemaji wa Sumaye... “Sitaki kumzungumzia Sumaye.

Mimi si msemaji wake. Tumsubiri yeye azungumze kuhusu hilo.” Kada wa CCM Hanang’ anena Katika hatua nyingine, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Hanang’, Goma Gwaltu amekionya chama hicho kuwa kisipodhibiti vitendo vya rushwa katika chaguzi zake, kitakufa. Gwaltu alisema jana kwamba kwa mazingira yaliyopo sasa ndani ya CCM bila hatua kali kuchukuliwa, kiongozi asiye na fedha hawezi kushika uongozi na ndiyo sababu anaungana na wana-CCM wengine katika wilaya hiyo, ambao wanafikiria kukihama chama hicho.

 “Kama wewe una nia ya kuendelea na siasa siyo rahisi kushinda hapa Hanang’ ukiwa hukubaliani na watu fulani, sasa mimi naona ni bora tu kutafuta chama kingine kwani siyo dhambi,” alisema Gwaltu bila kuwataja ambao wanataka kuhama CCM. Hata hivyo, Gwaltu alisema kwa upande wake, hafikirii kuendelea na mambo ya siasa wala kulalamika makao makuu ya CCM kuhusiana na alichokiita hujuma alizofanyiwa.

Kikwete Atembelea Canada

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Mhe. John Baird baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Macdonald Cartier jijini Ottawa, Canada, kwa ziara rasmi ya siku mbili jijini  humo Jumatano Oktoba 4, 2012
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika viwanja vya jumba la Rideau Hall jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya  kuanza ziara rasmi ya siku mbili jijini  humo Jumatano Oktoba 4, 2012. Jumba hilo ndilo makazi  na ofisi rasmi ya Gavana Jenerali wa Canada tangia mwaka 1867 ambapo pamoja na kuishi humo pia hapo ndipo hutumika kwa kuwatunukia wananchi wa Canada waliofanya vyema, pa kupokelea wageni mashuhuri wa nchi za nje na pia ndipo anapofanyia shughuli zote za kitaifa akiwa kama mwakilishi wa Malkia wa Uingereza.

Wednesday, October 3, 2012

Louise na Martine Malaya mapacha wa Masterdam

 
Makahaba hawa wameangaziwa kufuatia kutolewa kwa kumbukumbu zao na Filamu inayohusu maisha yao. Filamu hiyo, (Meet the Fokkens), inawaangazia Makahaba mapacha wenye umri wa miaka 70 Louise na Martine Fokken ambao walitufichulia siri yao katika kufanya ukahaba katika Mji maarufu zaidi kwa ufuska duniani.
Louise na Martine hutumia muda wao mwingi wakiwa kwenye Maskani yao ya vyumba viwili katika eneo la Ijmuiden, magharibi mwa Amsterdam. Huku wakiwa wamevalia viatu vya ndala, wao huranda randa hapa na pale chumbani wakinywa kahawa na kula keki wakionekana kukosa muelekeo.
Martine anaimba kwa sauti ya chini huku Louise akielezea masaibu yaliyoikumba familia yake na kumlazimu kukimbilia usalama wakati wa Vita vya pili vya Dunia.
Mama yao alikuwa na usuli wa Kiyahudi, jambo walilofanya kuwa siri kubwa kwa Wanajeshi wa Nazi waliokuwa wanashika doria nchini Uholanzi. Wimbo wa Louise uligusia Furaha na Huzuni za maisha.
"Tulikuwa watoto wadogo wakati huo wa vita. Ving'ora vilipoanza kulia, mama yetu alituficha katika eneo la chini ya nyumba. hatukuwa na kofia za chuma, hivyo basi tulitumia vikaango vya kupikia kukinga vichwa vyetu. Tulionekana kuchekesha na kana kwamba tunafurahia hali hiyo."
Nilimuuliza iwapo maisha wakati huo hapa Amsterdam, yalikuwa ya furaha au kuhuzunisha?
Makahaba mapacha Louise na Martine
Mapacha hao wanasema kutolewa kwa kumbukumbu zao kumebadilisha muelekeo wao; hapo mbeleni walitusiwa, sasa wanaheshimiwa "Oh ni kicheko, bila shaka ni kicheko. huna budi kucheka hata unapokuwa na huzuni kwa sbabu ni maisha yako na huwezi kuyabadilisha, lakini ni bora ukiwa unatabasamu kila mara."
Dada hao wawili wanatingisa vichwa vya ishara ya kuafikiana katika wanayoeleza.
Hata hivyo, tabasamu lao la kujilazimisha haliepuki kudhihirisha huzuni inayojitokeza machoni mwao.
"Bila shaka hatukuwaza kamwe tulipokuwa na umri wa miaka 14 au 15 kwamba siku moja tungejiingiza kwenye Ukahaba. Tulikuwa wabunifu na tulikuwa na Matarajio maishani" akadokeza Martine says.
Louise naye akaongezea: "kila siku mimi husema ni mume wangu aliyenipiga na kuniingiza kwenye ukahaba. Alikuwa mtu anayetumia mabavu na kutishia kutengana nami endapo ningekataa kufanya ukahaba ili kutafuta pesa.
"Yeye alikuwa kipenzi maishani mwangu…" akasema.
Wanawe Louise' hatimaye wakaishia kulelewa kwenye makao ya watoto. Alituonyesha mojawapo ya picha zilizopo kwenye rafu ya vifaa vya kale, inayodhihirisha nyuso zao zenye tabasamu.
Uzoefu wa miaka mingi
Martine bado anafanya Ukahaba. Anasema malipo ay uzeeni anayopata kutoka kwa Serikali ya Uholanzi hayamtoshelezi kujikimu kimaishai. Isitoshe anaugua ugonjwa wa Baridi yabisi.
Martine anasema ijapokuwa angependa kustaafu lakini hawezi kuendelea kujikimu kimaisha. Filamu inayomuhusu inamuonyesha akiwa kazini, amejipachika kwenye kiti akiwa amevalia soksi ndefu, mshipi na viatu vya kisigino.
Makahaba mapacha Louise na Martine
Martine Fokken ni kivutio kwa wanaume wakongwe badala ya vijana wanaompita bila hata kumtazama na kumkejeli kuwa amezeeka mno. Kama kawaida yake, anaangua kicheko na kusema hajali kamwe.
Anasema nyakati zimebadilika: "Vijana wa sasa ni tofauti, wanakunywa pombe sana, wamenona na hawakuheshimu. Wanapaswa kuwa kwenye pikipiki zao kama wavulana wa Kidachi badala ya kupoteza wakati wakinywa pombe."
Licha ya ushindani mkali kutoka kwa Vidosho wenye umri mdogo katika eneo la karibu, Martine hakosi wateja.
Anaonekana kuwavutia zaidi Wanaume wazee. Yeye hutumia vitu wanavyopendelea kuvaa ili kuwavutia kama vile kuingia kwenye madanguro akiwa na mjeledi huku amevaa viatu vya kisigino kirefu.
Chanzo: BBC